Bei

Lengo letu ni:kufanya what3words iweze kupatikana kila mahalikuwaunga mkono watu ambao wanafanya mambo mazuri duniani kotekuondoa vizuizi vinavyoweza kufanya what3words isienee kila mahali
Daima what3words haitalipishwa kwa watu kuitumia kwenye tovuti na programu zao, na daima kutakuwa na njia za kutumia furushi zetu za programu ya biashara bila malipo.

Tunachukua hatua hasa kuunga mkono matumizi ya haki na ya usawa ya teknolojia yetu msingi ya anwani, ikiwa ni pamoja na kutumia muundo wa ada ambao unapatia mashirika yanayostahili aina mbalimbali za mipango ya matumizi yasiyolipishwa na yaliyopunguzwa ada. Lengo letu ni what3words kuwa ndicho kiwango cha kimataifa cha kutoa maeneo, na tumechukua mfumo wa biashara ambao unatusaidia kufikia lengo hili.

Kwa hivyo, tuna matoleo ya aina mbalimbali ya kuhakikisha kuwa mashirika yanayojumuisha what3words yanaweza kuwa na uhakika katika upatikanaji wa muda mrefu wa teknolojia hii.

Zaidi ya hayo, tumejitolea kwa yafuatayo:

Ikiwa sisi, what3words ltd, tutashindwa kudumisha teknolojia ya what3words au tufanye mipango ya teknolojia hiyo kudumishwa na mhusika mwingine (mhusika huyo mwingine akiwa tayari kutoa ahadi hii), basi tutatoa msimbo chanzo wetu kwa umma. Tutafanya hivi kwa njia na leseni na stakabadhi zinazofaa ili kuhakikisha kwamba watumiaji wote wa what3words, iwe ni watu, biashara, mashirika ya ufadhili, mashirika ya kutoa misaada, serikali au mtu mwingine ataweza kuendelea kutegemea mfumo wa what3words.