Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Majibu ya maswali ya kawaida

Dunia hii si ina anwani za kutosha?

La. Karibu asilimia 75 ya ulimwengu (nchi 135) zina shida ya mifumo ya anwani isiyopatana, ngumu au isiyotosha. Kwa ujumla watu bilioni 4 duniani hawana anwani. Lakini hata kwa nchi ambazo anwani zinafanya kazi vizuri, bado haiko sawa. Kwa mfano, kuna Barabara nane tofauti za Lonsdale London; nyumba nyingi hazina nambari; anwani haiwezi kukueleza kiingilio sahihi cha jengo kubwa; ukiwa ng’ambo anwani inaweza kuwa ngumu kuelewa. Mara kwa mara unataka kuongea kuhusu mahali ambapo hapana anwani ya mtaa.

Iwapo utaweka pini kwenye simu yangu ya mkononi?

Kuweka pini kwenye simu yako hukuelezea vizuri mahali upo na kushiriki eneo hilio na mtu mwingine ambaye yuko kwenye programu hiyo ni rahisi sana. Hata hivyo hiyo hushughulika tu na ni wapo ulipo sasa hivi, haikusaidii kurejelea mahali tuli, au ikiwa mtu hatumii programu hiyo, au ikiwa mtu huyo hana muunganisho wa data, au ikiwa anataka kuikumbuka, au ikiwa anataka kutumia eneo hio katika programu nyingine.

Ninaweza kuitumia aje?

Ikiwa unataka kupata anwani ya 3 word ya eneo lako la sasa au la mahali pengine, unaweza kugonga kwenye kitufe cha nipate mimi ili ukaribie au utafute anwani ya mtaa, kisha unaweza kukuza ili uone gridi ya 3mx3m na usogeze ramani na pini ili upate mahali unapotaka. Kubadilisha kwa mwonekano wa setilaiti husaidia wakati unapokuza ndani.

Programu hii ina lugha ngapi?

Tumeanzisha mfumo wetu wa 3 word kwa lugha 8: Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiurusi, Kijerumani, Kiuturuki na Kiswidi. Tunaongezea lugha hizo kila mwezi na kwa sasa tunashughulikia Kiitaliano, Kiigiriki, Kiarabu, Kiswahili na zaidi.

Je, nitumie lugha gani?

Unaweza kutumia lugha yoyote kati ya hizo. Ikiwa wewe ni Mrusii na unataka kutumia what3words ili kuwaelezea Warusi wengine kuhusu anwani nchini Meksiko, unaweza kutumia верба.осенний.редька – mahali nje ya Mji wa Meksiko. Hivyo hivyo pia unaweza kuona anwani kwa Kiingereza, au Kihispania katika kitabu cha maelekezo. Unaweza kutumia lugha yoyote kati ya hizo. Unaweza kuchagua lugha ya 3 word ambayo itakuonyesha anwani za 3 word, lakini sio lazima utueleze ni lugha gani unaingiza anwani za 3 word: tutatambua lugha kiotomatiki.

Je, anwani ya 3 word kwa Kifaransa (au lugha nyingine yoyote) tafsiri ya anwani hiyo moja ya 3 Maneno kwa Kiingereza?

La: anwani ya 3 word kwa lugha moja sio tafsiri ya 3 Maneno inayotumiwa kwa toleo la lugha tofauti.

Na kuhusu maneno ya matusi, na maneno ambayo ni kama yanafanana?

Tumeondoa maneno ya kuchukiza na homofoni (k.m. sale na sail), na tumechanganya maeneo yetu yote ya 3 word yanayoonekana kufanana (k.m. kwa wingi) na tukayaweka mbali kabisa na kila moja kama iwezekanavyo ili dhahiri unapokosea. Ni bora kuwa umepotea maili 400 kuliko maili 1 ili ujue mara moja kuwa umekosa na usielekee mahali pasipofaa!

Je, ninahitaji kuwa na programu?

Unaweza kutumia kivinjari kwenye kompyuta yako, kompyuta kibao au simu maizi kugundua, kuingiza na kushiriki anwani ya 3 word. Programu ya what3words ina vipengele vingi vizuri sana, lakinio sio muhimu vile kwa kuwa unaweza kutumia tovuti ya what3words wakati wowote.

Je, wengine wanahitaji kuwa na programu nikiwatumia anwani ya 3 word?

Unaweza kutuma anwani ya 3 word kwa mtu yeyote, ukiwa na uhakika kwamba ikiwa mtumiaji anayepokea bado hana programu hiyo, anaweza bado kufikia eneo lako kupitia kompyuta yake, kompyuta kibao au kivinjari cha simu maizi.

Je, ni wapi ninaweza kutumia what3words?

Matumizi ya what3words ni tofauti. Makampuni ambayo kubainisha na kuwasiliana eneo sahihi ni muhimu sana wanajumuisha teknolojia yetu kupitia API na SDK yetu. Duniani what3words inajumuishwa kwenye mifumo ya uelekezaji, programu za car-share na tovuti za raslimali na hata pia kutumiwa na wasafirishaji mizigo, teksi na huduma za usafiri.

Je, ninaweza kuitumia na programu za uelekezaji kama vile Google & Waze?

Unaweza kubainisha anwani ya 3 word katika programu ya what3words au tovuti ya what3words, na kisha kwa kuchagua chaguo la uelekezaji, unaweza kufungua eneo hilio katika programu za uelekezaji zilizosakinishwa kwenye kifaa chako. Hii hujumisha Google Maps, Apple Maps, Waze na CityMapper.

Je, ninaweza kuicharaza kwenye ramani za Google?

Bado. Tuna programu na huduma kadhaa za ubia ambapo unaweza kuingiza anwani ya 3 word moja kwa moja kwenye kiolesura chao. Hivi karibuni tunatumaini wha3words itakubaliwa katika programu zote kuu duniani za ramani na uelekezaji.

Ninawezaje kushiriki au kutuma anwani ya 3 word?

Kubofya kwenye kitufe cha kushiriki katika programu au tovuti yetu hukuwezesha kutuma 3 Maneno kupitia SMS, barua pepe, mitandao ya kijamii na programu yoyote ya kutuma ujumbe uliyosakinisha. Unaweza pia kuinakili au kuwaelezea watu katika mazungumzo au kuiandika chini.

Je, programu hii inakubali urefu au shughuli za ndani?

Inatumika ndani, katika 2D, lakini sio 3D, k.m. urefu au mwinuko. Teknolojia husika (mkao wa ndani, ramani ya ndani, uelekezaji wa ndani) haijaenea bado vya kutosha ili kuwa na faida yoyote kubwa ya kubainisha eneo linalojumuisha urefu. Hata hivyo, ikiwa na wakati urefu itakuwa ya maana kubainisha, tuna chaguo mbalimbali za kujumuisha maelezo haya.

Je, unaweza kuitumia bila muunganisho wa data?

Ndiyo: mfumo wote wa what3words ni mdogo sana, na kwa hivyo unaweza kufanya kazi nje ya mtandao wakati mtumiaji hana muunganisho wa data. Programu ya what3words na programu na huduma za washirika wetu huzinduliwa kwa kawaida kwa kutumia toleo la mtandaoni la mfumo wetu, lakini usaidizi wa nje ya mtandao unajumuishwa katika programu zaidi na zaidi ambazo hutumia what3words (ikiwa ni pamoja na yetu).

Ni aje kuhusu latitudo na longitudo (viambatishi vya GSP)?

Tunapenda latitudo na longitudo na what3words inaitegemea. Tunachukua tungo hizo refu za nambari na herufi na kuzigeuza kuwa maneno matatu rahisi. Unahitaji dijiti 16, vibambo 2 (+/-/N/S/E/W), pointi 2 za desimali, na nafasi/koma/mstari mpya ili kubainisha eneo kwa usahihi wa mita 3 kwa kutumia viambatishi vya GPS. Hiyo ni nzuri kwa kompyuta na vifaa wakati wanadamu wanahusika, lakini wanadamu huwa wanahusika. what3words ni kiolesura cha wanadamu kwa latitudo na longitudo.

Je, maneno yatawahi kubadilika?

La: kwa sababu mfumo wa what3words ni wa kudumu, na haiwezekani kuubadilisha, kuna uhakika wa asilimia 100 kwamba matukio yote ya mfumo kuendeshwa mahali popote duniani utatoa anwani hiyo moja ya 3 word kwa eneo hilo moja. Usijali kuhusu kitu chochote kubadilika. Kimewekwa kudumu tayari na kitabakia hivyo. Ikiwa unataka kupata anwani ya 3 word ya mahali pengine kando na eneo lako la sasa, unaweza kutumia anwani ya mtaa kukaribia, lakini unastahili kukuza na usogeze ramani (jihisi huru kutumia mwonekano wa setilaiti) ili upate eneo sahihi.

Mfumo huu ni mkubwa kivipi? Trilioni 57 ni anwani nyingi sana!

Mfumo wote wa what3words ni MB5. Hii ni ndogo vilivyo kutoshea kwenye programu ili watumiaji waweze kutumia what3words wakati mtandaoni au nje ya mtandao k.m. hauhitaji muunganisho wa data ili kupata anwani yako ya sasa ya 3 word au kutafuta anwani ya 3 word uliyopewa.

Je, ni kwanini ulitumia maneno 3 badala ya maneno 2 au maneno 4?

Kugawa dunia katika miraba ya 3m x 3m (ambayo ni ndogo vilivyo kusaidia kwa malengo yote halisi) hukupa miraba trilioni 57 kwa hivyo… – Ukiwa na neno 1 unaweza kutaja miraba 40,000 ya 3m x 3m, kwa hivyo hiyo ni kila mraba 3m x 3m katika kijiji kidogo. Lakini dunia ni kubwa zaidi hii kwa hivyo utakuwaa mfumo usio na maana. – Kwa mfululizo wa maneno 2 unaweza kutaja miraba 1,600,000,000 ya 3m x 3m, kwa hivyo hiyo ni kila mraba 3m x 3m katika eneo lenye ukubwa wa Hawaii. Lakini dunia ni kubwa zaidi hii kwa hivyo utakuwaa mfumo usio na maana. – Kwa mfululizo wa maneno 3 unaweza kutaja miraba 64,000,000,000,000 ya 3m x 3m, kwa hivyo hiyo ni kila mraba 3m x 3m duniani (kwa hakika tuna michanganyiko michache ya ziada). – Kwa mfululizo wa maneno 4, tunaweza kutaja kila mraba wa 3m x 3m katika eneo kubwa mara 40,000 ya ya ukubwa wa dunia, lakini hakuna haja ya hiyo . Ikiwa mwanadamu ataishi kwenye jua hivi karibuni, kwa hakika tutaweza kuizidisha, kwa kubadilisha chapa kidogo tu.

Itakuwa aje nikiandika tahajia vibaya au niseme neno vibaya?

Wanadamu hufanya makosa – makosa mengi sana. Mfumo wetu umeboreshwa kugundua na kusahihisha kiotomatiki makosa ya anayeshiriki na anayepokea. Mfumo wa kusahihisha otomatiki wa what3words huchukua hitilafu katika tahajia, kuongea, na kutosikia maeneo ya 3 word. Tumechanganya maeneo yetu yote yenye 3 word zinazofanana na kuziweka mbali sana na eneo lingine kama hilo, kwa hivyo tunaweza kutumia eneo lako kukisia kwa werevu ulimaanisha nini. Wakati mwingine na anwani za mitaa, anwani zinazoonekana zinafanana zimekaribiana sana na inaweza kuchanganya sana na kusababisha kuchelewa wakati mtumiaji anapojaribu kufahamu ni nini kibaya kilichofanyika na anwani sahihi ni gani.

Je, inagharimu pesa ngapi?

Mfumo wetu msingi wa 3 word hautalipishwa kwa matumizi ya kibinafsi. Unaweza kusoma zaidi katika sera yetu ya bei.