Mercedes-Benz yaanzisha mfumo wa kwanza duniani wa urambazaji unaotumia sauti wa anwani ya maneno 3

Mercedes-Benz imetangaza mipango yake ya kuwa mtengenezaji wa kwanza wa magari kuzindua mfumo wa urambazaji wa anwani ya maneno 3.

Tangazo hilo linafuatilia ushirikiano na Daimler pamoja na mfumo bunifu wa anwani wa what3words.

what3words ni mfumo wa anwani wa kimataifa ambao umegawanya dunia kwa miraba ya 3m x 3m, kila mmoja ukiwa na anwani ya kipekee yenye maneno 3 ya kamusi. Kwa mfano, anwani ya maneno 3 ///genau.freundin.tagebuch, hurejelea mlango halisi wa kiwanda cha utengezaji Mercedes-Benz wa 3m x 3m kule Stuttgart-Untertürkheim.

Kiwanda hiki cha kutengeneza magari ya kifahari kimeunda wha3words kwenye mfumo wake wa burudani wa magari yake mapya unaozinduliwa mwaka ujao. Madereva wataweza kuandika au kusema maneno 3 ili kubaini mwisho halisi wa safari yao mahali popote duniani. Mfumo huu umeundwa katika gari la maonyesho lililo katika Maonyesho ya Magari ya Frankfurt.

what3words huondoa matatizo mengi ambayo madereva hukabiliana nayo wakitumia sauti ili kuingiza anwani za kawaida za mitaa na ni mfumo wa kwanza wa anwani ulioundwa ili kutumia sauti.

Faida kwa wateja wa Mercedes-Benz zipo wazi: anwani za maneno 3 ni thabiti zaidi kuliko anwani za mitaa au nambari za posta, hiyo huwawezesha madereva kurambaza kwa usahihi hadi kwenye mlango mahsusi wa jengo au eneo la kuegeshea magari. Mfumo huo pia unatumika kila mahali duniani, na unaweza kutumika kwenda kwenye bustani, ufukoni, na sokoni – kwa hivyo madereva wanaweza kufurahia maeneo mbalimbali ya mijini na mashambani ambayo hayana anwani zozote za mitaa.

Katika tafiti za hivi karibuni za wamiliki wa magari mapya, JD Power aligundua kwamba ugumu na mifumo isio sahihi ya urambazaji wa magari ndio tatizo linaloripotiwa sana*. Mercedes-Benz inajivunia kuongoza katika kutatua tatizo ambalo tasnia hii kwa ujumla imesumbukana nalo kwa muda mrefu.

‘Mbinu yetu kuhusu HMI imelenga kabisa kuwapa wateja wetu uzoefu bora, rahisi na wenye starehe kabisa alisema Said Sajjad Khan, makamu wa rais wa Digital Vehicle and Mobility, Daimler AG. ‘Anwani za maneno 3 ni rahisi sana kutumia, kumaanisha madereva wanaweza kusema eneo lolote kwenye magari yao, na wawe na uhakika kwamba wanaelekea eneo sahihi, kila wakati’. .

‘Anwani za kawaida za mitaa hazikuundwa kutumia sauti’ alisema Chris Sheldrick, CEO na mwanzilishi mwenza wa what3words. ‘Barabara ya 15 Ammanford na Barabara ya 50 Ammanford ni ngumu kwa mfumo wa sauti kutofautisha na majina mengi ya nyumba na ya barabara si ya kipekee. Kuna Barabara 14 tofauti za Church Road Uingereza, na Mitaa 632 ya Juarez katika Mji wa Meksiko. Anwani za mitaa hutumia pia maelfu ya maneno yasiyo kwenye kamusi, ambayo matamshi yake yanaweza kuwa magumu kuyakisia. Mji wa Godmanchester, unatamkwa ‘Gumster’. Mercedes-Benz inajulikana kwa uvumbuzi, kwa hivyo haitushangazi kwamba ndio kampuni ya kwanza ya magari kujumuisha mfumo wetu katika magari yake’.

Wakati dereva anapoingiza anwani ya maneno 3 kwa kutumia sauti au maandishi, teknolojia ya what3words huigeuza kuwa kiwianishi. Kisha gari hutafuta eneo hili sahihi kwa kutumia mfumo ulioundiwa ndani wa ramani na urambazaji. what3words inapatikana sasa kwa lugha 14, lugha zaidi zinaendelea kutengenezwa, inayowaruhusu watu kusema anwani ya maneno 3 kwa lugha yao asili ili kuingiza mwisho wa safari yao, haijalishi ni wapi duniani.

* Chanzo: JD Power

Jua zaidi kuhusu kutumia what3words kwa Magari na Uchukuzi

what3words huwezesha

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia what3words katika biashara yako:

By asking us to get in touch you are agreeing to receive communications from us as described in our privacy policy