Kuhusu

what3words ni mfumo wa kutoa anwani ulimwenguni. Tumegawanya ulimwengu katika miraba ya 3m x 3m na tukaupa kila mraba anwani ya kipekee ya maneno 3. what3words hutoa njia sahihi na rahisi sana ya kuzungumza kuhusu maeneo. Na humaanisha kila mtu na kila mahali sasa pana anwani.

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia what3words katika biashara yako:

Si ulimwengu tayari una anwani?

Anwani ulimwenguni hazifai mahitaji ya kila siku. Anwani za mitaa zinaweza kuwa si sahihi au zenye utata. Majina ya barabara yanarudiwa rudiwa. Mara kwa mara nyumba na biashara huwa mbali na kituo cha msimbo wake wa posta. Na maeneo mengi ya ulimwengu hayana anwani – kuanzia vitongoji duni vya mji na mitaa ya mabanda hadi bustani ambapo umepanga kukutana na marafiki, au eneo sahihi ambapo unasubiri teksi ikuchukue.

Kuishi nje ya mtandao

Umoja wa Mataifa (UN) unakadiria kuwa watu bilioni 4 wanakosa njia ya kuaminika ya kuzipa nyumba zao anwani. Hivyo basi, wananyimwa huduma msingi za kijamii na umma. Wanasumbuka kufungua akaunti za benki, kujiandikisha kuzaliwa au kupata huduma za umeme au maji. Bila uwezo wa kusema wanakoishi, watu hawa wanakuwa hawaonekani na serikali.

Hailingani na dhumuni

Anwani duni humaanisha bidhaa hupotea, biashara haziwezi kupatikana, msaada haufiki, inakuwa vigumu kusimamia mali iliyo mbali na marafiki hushindwa kukutana. Wakati inafanya kazi, ni ghali na inakatisha tamaa. Wakati haifanyi kazi, huzuia ukuaji na maendeleo, huzuia uwezo wa jamii kutembea na huathiri maisha.

Mfumo wa anwani haulingani na si kamili

Asilimia 75 ya ulimwengu una matatizo ya anwani duni au hakuna anwani hata kidogo. Asilimia 25 iliyosalia bado inakosa anwani inayokubalika kote. Ijapokuwa maboresho yamefanywa katika ramani na urambazaji, kuelezea ni wapi “pale” kumesalia kuwa tatizo kuu kabisa.

Fursa nyingi

Tasnia ya maeneo ya jiografia ina thamani ya hadi dola bilioni 150 kila mwaka. Urejeleaji wa maeneo sahihi na thabiti hakuboreshi tu anwani za ulimwengu, bali kunaweza pia kukuunganisha na wateja ambao hawajafikiwa na sekta mpya za viwanda. Mara tu watu wanapogundua vikwazo vya mbinu za sasa za anwani, wanaona jinsi anwani za maneno 3 zinaweza kuwa majibu ya matatizo mengi.

Kutumia what3words katika biashara yako

what3words inapatia kila mtu na kila mahali anwani ya maneno 3. Ni sahihi, rahisi na ya kipekee. Na inabadilisha jinsi watu na biashara wanavyozungumza kuhusu eneo.

Maneno yanazidi nambari

Kutumia maneno kunamaanisha kuwa watu wasio wa kiufundi wanaweza kugundua na kuelewa anwani ya maneno 3 kwa urahisi zaidi kuliko msimbo wa posta au viwianishi vya GPS. Pia wanaweza kushiriki anwani hiyo kwa haraka zaidi, kwa usahihi zaidi na bila utata wowote ikilinganishwa na mfumo wowote mwingine.

Rahisi kukumbuka na kutumia

Mfumo wa what3words unatumia orodha ya hadi maneno 40,000, kulingana na toleo la lugha unalotumia. Algorithimi inaainisha orodha hii ili maneno rahisi na ya kawaida zaidi yanatumiwa katika maeneo yenye watu wengi zaidi, huku maneno marefu yakitumiwa katika maeneo yasiyo na watu wengi.

Watu nyuma ya what3words

what3words iliundwa kwa sababu anwani ulimwenguni haitoshi kwa mahitaji ya kila siku. Chris Sheldrick, ambaye awali alikuwa katika tasnia ya muziki, aligundua hitaji la mfumo bora wa anwani, baada ya bendi na vyombo kupotea mara kwa mara.

Chris alitafuta usaidizi wa marafiki wawili, Jack Waley-Cogen na Mohan Ganesalingam, ili kubuni algorithimi msingi, kutengeneza orodha ya kwanza ya maneno na kuunda app na tovuti. Hawa watatu walishirikiana kuanzisha what3words katika mwaka wa 2013 na bado ndio nguzo ya kampuni hii.

Timu hii imekua na sasa ina idara nne msingi – Ukuzaji Biashara, Lugha, Bidhaa na Uuzaji. Kampuni hii inaendelea kukua, kwa utaalamu na uzoefu, ukuzaji bidhaa, uwekezaji na kukubaliwa.

what3words huwezesha

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia what3words katika biashara yako:

By asking us to get in touch you are agreeing to receive communications from us as described in our privacy policy