Kwenda ngazi za kimataifa pamoja na what3words na Aramex

Mfumo wa sasa wa kutoa anwani duniani hautoshi. 75% ya nchi zina matatizo ya mifumo duni au isiyokuwepo ya anwani. Na kwa asilimia 25 ambayo ina anwani thabiti, mizigo bado hupotea, wasafirishaji mizigo wanapotea njia na biashara za ndani haziwezi kupatikana.

Jambo linastahili kufanywa ili kufanya mfumo wa anwani kuwa bora zaidi.

Suluhu la maneno 3

what3words ni mfumo wa anwani ambao ni sahihi na pia rahisi. Inatumia gridi ya dunia ya miraba ya 3x3m, inayopangia kila mraba anwani ya kipekee ya maneno 3.

Ni sahihi zaidi kuliko anwani ya posta na inayoweza kukumbukwa kwa urahisi zaidi kuliko viwianishi vya GPS. Inamaanisha watu wanaweza kubainisha eneo fulani kwenye sayari na kulielezea kwa haraka na urahisi zaidi kuliko mbinu nyingine yoyote. Mfumo huu unasaidia kuimarisha biashara, kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na mwishowe kuokoa maisha.

Kufanya ‘Maili ya Mwisho’ kuwa muhimu

Mojawapo ya changamoto kubwa zinazokumba makampuni usafirishaji ya kimataifa ni kupata njia wastani ya kupata na kuthibitisha maeneo ambako bidhaa zinafikishwa. Mifumo ya anwani ya kitaifa inatofautiana kulingana na nchi na kwa kawaida huwa haitoshi. Mifumo ya urambazaji inayotegemea GPS ni thabiti, sahihi na inayofaa mashine lakini ni ngumu kuelewa na inaweza kukabiliwa na hitilafu za kibinadamu.

Hapo ndipo what3words inaweza kuleta tofauti, na sababu kampuni kubwa ya kimataifa ya usafirishaji, Aramex, sasa inatumia mfumo huu katika kutimiza operesheni zake za biashara ya mtandao. Ujenzi wa anwani ya maneno 3 huwa thabiti kila wakati, iwe mzigo unapaswa kusafirishwa hadi pwani mwa Afrika au katikati mwa Asia. Na kila anwani ya kipekee inaweza kutumiwa na programu ya ufuatiliaji na hata pia madereva wa kufikisha.

Aramex inalenga kutumia anwani za maneno 3 kuimarisha pakubwa ufikishaji muhimu wa ‘Maili ya Mwisho’, ambayo inawajibika kwa karibu asilimia 28 ya gharama za jumla za ufikishaji. Bila anwani sahihi au eneo maalum, mara kwa mara madereva hulazimika kuendesha wakijaribu kupata wanakoelekea, au wanalazimika kusitisha ufikishaji huo.

Kinyume na hiyo, anwani ya maneno 3 inamaanisha dereva wa ufikishaji anaweza kubainisha eneo la kufikisha hadi kwa mraba wa kipekee wa 3x3m, mahali popote duniani. Na hiyo inamaanisha bidhaa zinawasili maeneo yake yaliyokusudiwa mara ya kwanza, na kwa wakati unaofaa.

“Tunafurahia kushirikiana na what3words”, alisema Hussein Hachem, Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) wa Aramex. “Kwa kujumuisha anwani za maneno 3 katika operesheni za biashara yetu ya mtandaoni barani Mashariki ya Kati, Afrika na Asia, tunaweza kuwafikia vyema wateja zaidi kote duniani, hata wale walio katika maeneo ambayo ni magumu kufika”. cqwhpykwyaaagjn

what3words na wewe

Bila miundomsingi ya mfumo sahihi wa anwani, ufikishaji na usafirishaji unakuwa wenye changamoto na pia unagharimu sana. Kila dakika ya ziada inayotumika kutafuta anwani ya makazi, au eneo la kuchukua au eneo maalum ni muda na pesa ambazo zitaathiri faida zako.

Kwa watu walioathirika, ukosefu wa anwani thabiti inamaanisha muda uliopotezwa wa kusubiri wasafirishaji kuwasili, kukata tamaa kwa kulazimika kutoa maelekezo kwenye simu na, katika hali nyingine, mizigo haifiki kabisa.

Ushirikiano wetu na Aramex ni mojawapo ya njia nyingi ambazo tunasaidia makampuni ya usafirishaji na ufikishaji – katika ngazi za ndani, kitaifa na za kimataifa – kuimarisha operesheni zao.

Jua mengi zaidi kuhusu kutumia what3words kwa Ufikishaji, Usafirishaji na Biashara ya Mtandaoni

what3words huwezesha

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia what3words katika biashara yako:

By asking us to get in touch you are agreeing to receive communications from us as described in our privacy policy