Land Rover inashirikiana na what3words ili kutoa mwelekeo mpya wa uendeshaji gari nje ya barabara kwa kutumia app ya ARDHI

Land Rover inashirikiana na what3words ili kutoa anwani sahihi za maneno 3 kwa app yao ya simu maizi ya ARDHI ya uendeshaji gari nje ya barabara.

Pamoja na app ya ARDHI ya uendeshaji gari nje ya barabara, matukio huanza wakati barabara inapofika mwisho. Madereva wanaweza kupanga njia mpya, kusafiri njia ambazo ziliundwa na wengine, kukadiria njia kulingana na ugumu na kupata beji za hatua walizofanikisha barabarani.

App hii tayari ina maelfu ya njia zilizopangwa katika mandhari yote ya Mashariki ya Kati na Afrika – kuanzia vyungu vya mchanga vya Dubai hadi safu ya milima ya Atlas ya Moroko kule Afrika Kaskazini. Pia inahusisha mipasho ya hali ya hewa na hata pia uwezo wa kutuma “mwako” ili kuwavutia madereva walio karibu iwapo kuna hali ya dharura.

Kukiwa na njia nyingi sana zinazowapeleka madereva katika himaya isiyo na ramani, app ya ARDHI inahitaji njia thabiti na sahihi ya kutambua na kuelezea eneo. Ijapokuwa GPS inaweza kutoa kiwango hicho cha usahihi, ni vigumu kutumia viwianishi na vinaweza kukabiliwa na makosa wakati wa kuvishiriki na wengine. Kama suluhu, app ya ARDHI imejumuisha what3words kwenye mfumo wake. Mfumo wa anwani wa ‘what3words’ unategemea gridi ya dunia ya miraba trilioni 57 ya 3m x 3m. Kila mraba umepangiwa mapema anwani ya kipekee ya maneno 3. Inatoa kiwango sawa cha usahihi kama viwianishi vya GPS lakini ni rahisi zaidi kukumbuka na kushiriki.

Madereva wanaweza kuweka anwani za maneno 3 kwenye programu ya ARDHI, ili watumie kama njia ya wanakoelekea au njia za kupitia barabarani. Inamaanisha wanaweza kwenda nje ya barabara hadi himaya isiyojulikana na bado wapange kukutana na marafiki katika kituo cha kupiga kambi kilicho revised.bonuses.cheeses kule Umm Al Quwain, au kuchunguza ufuo uliotengwa wa Khasab kutoka lectured.harpoon.just Iwapo dereva atakuwa na matatizo yoyote basi anaweza kutumia anwani ya maneno 3 kutambua eneo lake sahihi, linalolingana na mraba wa 3m x 3m. Inamaanisha madereva wengine katika eneo hili – au magari ya usaidizi na ya dharura – wanajua ni wapi hasa wataenda kutoa usaidizi. what3words hata inafanya kazi bila muunganisho wa intaneti au mawimbi ya simu – muhimu kwa uendeshaji gari hadi maeneo yaliyo mbali na ustaarabu.

what3words inatumika katika zaidi ya nchi 170. Inasaidia makampuni ya kufikisha bidhaa kwa kutumia magari na droni, huduma za posta, makampuni ya usafirishaji, miongozo ya usafiri, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO) na kila mtu anayehitaji kupata au kushiriki eneo sahihi.

“Hadithi ya kweli ya nchi inapatika mahali barabara zinapofika mwisho,” alisema Mohammed Jaradat, Meneja wa Uuzaji wa Jaguar Land Rover ya Mashariki ya Kati. “ARDHI ndio app ya kwanza duniani ya uendeshaji gari nje ya barabara, inayowapa madereva njia ya kugundua barabara mpya na kushiriki njia hizo zao na ulimwengu. what3words inakupa rafiki kamili wa uendeshaji gari, anayetoa usahihi wa kubaini eneo, mahali popote safari itatupeleka.”

“Mashariki ya Kati ni eneo lenye nafasi nyingi na lenye ugunduzi,” alisema Chris Sheldrick, Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) na mwanzilishi mwenza wa what3words. “App ya ARDHI inaonyesha thamani hii, kwa kuunganisha hisia hiyo ya matukio pamoja na teknolojia ya hali ya juu. Ninatazamia kutumia ARDHI wakati ujao nikiwa katika eneo hilo, ili kutengeneza njia chache mpya zangu mwenyewe.”

Jua mengi zaidi kuhusu kutumia what3words kwa Magari na Uchukuzi

Use ARDHI

The ARDHI app from Land Rover has every feature you need to get the most out of your off-road experiences – from recording your unique paths on the map to sharing memories with friends and even earning bragging rights with badges.

ARDHI inapatikana kwa iOS & Android

Magari

what3words huwezesha

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia what3words katika biashara yako:

By asking us to get in touch you are agreeing to receive communications from us as described in our privacy policy