Kutambua maeneo ya majanga kwa kutumia what3words pamoja na Shirika la Msalaba Mwekundu la Filipino

Shirika la Msalaba Mwekundu la Filipino linatoa usaidizi na msaada muhimu wakati wa majanga, kama vile wakati wa mafuriko na vibunga vikubwa kote katika eneo la Filipino.

Kituo cha Operesheni kinatoa huduma ya udhibiti na uratibu saa 24 kwa siku na siku 7 kwa wiki kwa timu zinazofanya kazi katikati mwa maeneo ya majanga. Wanawajibika kutuma, kuhamasisha na kuwafuatilia watu na magari katika maeneo haya.

Katika kutambua maeneo sahihi, tayari nchi ya Filipino ina matatizo ya mfumo adimu wa anwani za mitaa na majengo. Hii imekithiri sana katika maeneo ya mashambani, ambako watu wanalazimika kuelezea eneo kulingana na minara iliyo karibu.

Katika maeneo ya majanga, anwani za kimaelezo kwa ufupi si fanisi. Huenda majengo yamebomolewa, barabara zimeporomoshwa na maji nazo alama za barabarani zimeharibika. Kuna uwezekano wa viungo vya mawasiliano kuharibika, kwa hivyo kuifanya iwe vigumu sana kushiriki data za maeneo kupitia intaneti.

Katika hali hizi za dharura Shiriki la Msalaba Mwekundu la Filipino limegeukia what3words, ili kutoa suluhisho thabiti na sahihi zaidi la anwani. Kwa kutumia anwani ya maneno 3, wahudumu nyanjani wanaweza kuwasilisha kwa ufanisi mahali ambapo msaada unahitajika, kupitia kusema au SMS rahisi.

Kituo cha Operesheni kinaweza kupanga usaidizi wa ziada kwenye eneo hilo, na kutuma wahudumu wa ambulensi au timu za utafutaji na uokoaji kwa haraka na urahisi zaidi.

Mfumo wa what3words pia unafanya kazi nje ya mtandao, kumaanisha timu zinaweza kushiriki maeneo yao bila kuhitaji muunganisho wa intaneti. Na huku magari mengi ya usaidizi yakikosa satnavs za GPS, kwa kutumia anwani ya maneno 3 pia kunahakikisha kuwa madereva bado wanajua wanakoenda. “what3words imekuwa zana muhimu katika kutusaidia kutambua maeneo ya majanga kwa haraka na kupanga timu za uokoaji,“ alisema Richard Juico Gordon, Mwenyekiti wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Filipino. “Kwa mfano, ilionekana kuwa ya maana sana katika kutusaidia kukabiliana na Kibunga kikubwa cha Haima mnamo Oktoba 2016.”

Kando na kukabiliana na majanga kwa haraka zaidi, timu ya Msalaba Mwekundu pia inatumia anwani za maneno 3 kuhifadhi maeneo ya rasilimali muhimu katika eneo hili – shule, hospitali, vituo vya uhamishaji. Katika matukio ya majanga ya siku zijazo, data hii itakuwa ya thamani sana, itakayohakikisha kuwa timu zinazotumwa zinajua mapema maeneo sahihi wanakohitajika kwenda. https://www.youtube.com/watch?v=bespLDjn6dU Kwa kuwa anwani za maneno 3 ni za kudumu na za kipekee, zinaweza kupatikana bila utata. what3words inatumiwa na wateja, makampuni ya uwasilishaji, zana za urambazaji, serikali, makampuni ya usafirishaji, miongozo ya usafiri na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali NGO). Pia inatoa maelezo ya maeneo kwa UN-ASIGN, programu ya kuripoti majanga ya shirika la Umoja wa Mataifa.

Jua mengi zaidi kuhusu kutumia what3words kwa Huduma za Dharura

what3words huwezesha

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia what3words katika biashara yako:

By asking us to get in touch you are agreeing to receive communications from us as described in our privacy policy