what3words ina ubia na kampuni kubwa ya usafiri ya Deutsche Bahn

what3words, jukwaa la kutoa anwani ulimwenguni lililojishindia matuzo mengi, limeshirikiana katika uwekezaji pamoja na Deutsche Bahn, kampuni ya pili kubwa zaidi ulimwenguni ya usafiri, na mwendeshaji reli na mmiliki mkubwa zaidi wa miundombinu barani Ulaya. Hii itasaidia matumizi endelevu ya what3words kote katika tasnia za usafirishaji na usafiri kote ulimwenguni.

Ubia huu una msingi wa uwekezaji kutoka kwa DB Digital Ventures, mpango mpya wa kimpangilio wa uwekezaji wa kimkakati wa Deutsche Bahn katika suluhu zinazochipuka za kusafiri na usafiri. Ikiwa na mipango ya kuwekeza Euro milioni 100 kama mtaji wa biashara kati ya sasa na 2019, DBDV inatenda kama mfadhili na mkuzaji wa mifumo mipya ya biashara ambayo itasaidia kuendesha bidhaa na huduma za siku zijazo za Deutsche Bahn.

Huku DB Digital Ventures ikiangazia siku zijazo za usafirishaji na usafiri, watakuwa wanakuza matumizi ya anwani za maneno 3 katika fursa mbalimbali kote katika vipengee vya biashara vya Deutsche Bahn Group.

DB Group inaendesha shughuli kote katika nchi 130, na ina zaidi ya waajiriwa 300,000, theluthi moja ya hao wakiwa nje ya Ujerumani. Kampuni hii iliwasafirisha watu bilioni 4.4 kote katika mitandao yake ya reli na mabasi ulimwenguni katika 2016. Katika kitengo cha Usafirishaji na Usafiri takriban tani milioni 300 zinasafirishwa kupitia reli na zaidi ya mizigo milioni 102 ikisafirishwa ardhini kila mwaka katika mtandao wa Ulaya. Katika mitandao ya kote ulimwenguni tani milioni 1.1 ya mizigo inayosafirishwa kwa ndege na karibu TEU milioni 1.9 ya mizigo inayosafirishwa kwa meli.

“Kuna hitaji wazi la usahihi unaotolewa na mfumo wa what3words, huku masoko ya ulimwenguni yenye anwani bora zaidi yakikubali teknolojia zinazohitaji usahihi wa juu zaidi kuliko unaotolewa na anwani za mtaa. what3words imeonyesha mtazamo kweli wa kiulimwenguni kupitia ubia walio nao na kiwango cha ukuaji na ubunifu kwenye miezi 6 iliyopita umekuwa wa ajabu,” alisema Boris Kühn, Mkurugenzi Msimamizi katika Deutsche Bahn Digital Ventures. “Usahihi na urahisi wa anwani za maneno 3 utasaidia vipengee vyetu vya biashara kuwa fanisi zaidi na kuendesha usasa kote katika mtandao wetu; cha muhimu zaidi, utatusaidia kuwasilisha suluhu za karne ya 21 za kusafiri na usafiri kwa watumiaji kote ulimwenguni.”

what3words kwa haraka inakuwa suluhu muhimu kwa mashirika ya urambazaji na usafiri kote ulimwenguni. Katika masoko kama vile Ulaya na Marekani, wasafirishaji wanatumia anwani za maneno 3 ili kuokoa muda katika kila uwasilishaji. Watumiaji wanatumia anwani za maneno 3 ili kukutana na marafiki, kupata matukio na kugundua maeneo muhimu yaliyojificha mijini – kuanzia maeneo ambayo hayana anwani katika bustani au fuo, hadi viingilio ambavyo ni gumu kuvipata vya Airbnbs au mabweni ya vijana. Anwani za maneno 3 pia zinatumiwa kuleta usahihi wa hali ya juu wa maeneo kwenye teknolojia za hali ya juu za kusafiri. Hivi majuzi mfumo huu uliwekwa kwenye mifumo ya uwasilishaji kwa kutumia droni inayotumia GoPato na Hylio, saa maizi na vifaa vya IoT kama vile saa maizi ya Blocks na kifaa cha urambazaji cha Beeline. Anwani za maneno tatu pia zimewekwa kwenye app ya nje ya barabara ya Ardhi ya Jaguar Land Rover na Next Future Transportation, wawasilishaji magari. what3words pia ni sehemu ya Start-up Autobahn, mpango wa Daimler / Porsche.

“Mifumo ya kutoa anwani iliyobuniwa miaka mamia iliyopita haina uwezo katika namna tunavyoishi leo. Anwani za mtaa si sahihi, na zinasababisha mkanganyiko mkubwa katika maeneo makubwa yenye viingilio vingi na maeneo mengi muhimu. Maeneo ya mashambani na majengo mapya katika miji inayopanuka kwa haraka yana anwani zisizo thabiti na wakati mwingine bila anwani kamwe,” alisema Chris Sheldrick, mwazilishi mweza na CEO wa what3words. “Kuokoa tu dakika mbili za muda wa kuwasili kunaweza kuokoa mamilioni ikiwa wewe ni mwendeshaji usafiri, na kunaweza kuokoa maisha ikiwa wewe ni mkabilianaji na matukio ya dharura. what3words inatoa usahihi wa anwani unaohitajika kwa teknolojia za siku zijazo – kuanzia magari ya kujiendesha hadi droni.”

what3words itatumia uwekezaji huu mpya miongoni kwa mingine ili kuimarisha bidhaa yao ya ugunduaji sauti ili kuwezesha magari kurambaza moja kwa moja hadi kwenye anwani za maneno 3 kwa lugha kadhaa kuu.

Jifunze mengi zaidi kuhusu kutumia what3words katika biashara yako

what3words huwezesha

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia what3words katika biashara yako:

By asking us to get in touch you are agreeing to receive communications from us as described in our privacy policy